Yanayojiri

SOKA:Francesco Totti aachana na AS Roma kama mkurugenzi wa ufundi.CECAFA:Simba SC na Yanga SC zajiondoa kushiriki Kagame Cup 2019 nchini Rwanda.CECAFA:TP Mazembe, DC Motema Pembe, AS Vita Club na Zesco United kushiriki Kagame Cup 2019 nchini Rwanda.AFCON 2019:Kundi A DR Congo,Misri, Uganda, Zimbabwe. Kundi B Burundi, Guinea, Madagascar, Nigeria. Kundi C Algeria, Kenya, Senegal, Tanzania. Kundi D Ivory Coast, Morocco, Namibia, Afrika Kusini. Kundi E Angola, Mali, Mauritania, Tunisia. Kundi F Benin, Cameroon, Ghana, Guinea-Bissau. CECAFA: Tanzania mwenyeji wa CECAFA Senior Challenge Cup 2019 Wanawake.CECAFA: Kenya mwenyeji wa CECAFA 2019 U-17 Wanawake. CECAFA: Uganda kuandaa CECAFA Senior Challenge Cup 2019.CECAFA::Eritrea kuandaa CECAFA Challenge Cup 2019 ya U-17.CECAFA:Rwanda mwenyeji CECAFA Kagame Cup 2019.CECAFA:Uganda mwenyeji CECAFA Challenge Cup 2019 ya U-20 Wanawake.

Magongo Rangers na Bandari Youth waanza kwa sare msimu mpya FKF Mombasa Premier League

Na Anthony Aroshee

Jumanne, Oktoba 8, 2019

Magongo Rangers FC na Bandari Youth FC walianza msimu mpya 2019/2020 wa Mombasa Premier League ya Shirikisho la Kabumbu nchini Kenya FKF tawi dogo la Mombasa kwa kutoka sare ya kufungana bao 1-1 katika mechi ya ufunguzi iliyofanyika Jumamosi iliyopita kwenye Uwanja wa Bomu huko Changamwe Kaunti ya Mombasa.

Vijana wa kocha Daniel Lenjo Bandari Youth FC, ndio waliotangulia kufunga bao la kuongoza baada ya mshambuliaji Ian Benjamin Okoth kufumania wavu wa Magongo Rangers FC dakika ya 70 akimalizia mpira wa krosi uliochongwa na beki wa kushoto aliyepanda, Abdulmajid Kadim.

Magongo Rangers FC walirudisha bao hilo dakika 10 baadae kupitia Said Suleiman ‘Daco’ aliyefunga kwa njia ya mkwaju wa tuta baada ya beki mmoja wa Bandari Youth kuunawa mpira ndani ya eneo la hatari.

Na kuhusu matokeo ya mechi nyingine zilizopigwa Jumapili iliyopita, timu ya Golden Boys FC kutoka Mikindani ilianza vyema msimu mpya kwa kupata ushindi wa nyumbani baada ya kuwatandika wageni Crossroads FC kutoka maeneo ya Nyali mabao 2-0 katika mechi iliyochezwa kwenye Uwanja wa shule ya msingi ya Kwa Shee.

Bao la kwanza la Golden Boys FC lilifungwa na Ian Kishao dakika ya 81 kabla ya Gabriel Otieno kuhitimisha ushindi huo kwa kupachika kimyani bao la pili na la ushindi dakika tatu baadae.

Wenyeji Zaragoza FC kutoka Likoni walianza msimu mpya wa FKF Mombasa Premier League kwa kupoteza nyumbani walipokubali kichapo cha mabao 2-0 kutoka kwa wageni Bamburi United FC ya Kisauni katika mechi iliyofanyika Masoud Mwahima Stadium.

Nayo Change Youth FC kutoka Likoni ilianza vizuri ikiwa nyumbani baada ya kupata ushindi mdogo wa bao 1-0 dhidi ya Tononoka Sports FC kwenye Uwanja wa Panama wakati Coolchester FC ikiishinda Annex FC mabao 3-2 kwenye Uwanja wa Mwembeni Wayani huko Changamwe.

Wanderers FC kutoka kisiwani Mombasa waliwanyoosha Nyali Youth FC kwa kuwabamiza mabao 3-1 katika Uwanja wa Tononoka huku wenyeji Westham FC wkitoka sare ya bao 1-1 dhidi ya wageni Junda Strickers FC kwenye Uwanja wa Ziwani Lasco.

KCN Poly FC walilazimishwa kutoa sare nyumbani ya bao 1-1 na Soweto FC katika Uwanja wa Mombasa Technical Training Institute MTTI(Bomani) nayo. Nayo Mantubila FC walipata ushindi wa bwerere wa alama tatu na mabao mawili bila kugusa mpira baada ya wapinzani wa Umba Sports Club FC kutoka Magongo kukosa kufika kwenye Uwanja wa Mantubila huko Shanzu.

Ligi hiyo itaendeea tena mwishoni mwa juma hili.

Msimu huu mpya 2019/2020 wa FKF Mombasa Premier League, unashirikisha jumla ya timu 18. Timu tatu Change Youth FC, KCN Poly FC na Tononoka Sports FC zinashiriki kwa mara ya kwanza katika ligi hiyo baada ya kupandishwa Daraja kutoka ligi Daraja la Kwanza msimu uliopita.

Chapa Barua pepe

Share

Dula - Bila wewe

Kocha wa Bandari FC Twahir Muhidin