Yanayojiri

SOKA:Francesco Totti aachana na AS Roma kama mkurugenzi wa ufundi.CECAFA:Simba SC na Yanga SC zajiondoa kushiriki Kagame Cup 2019 nchini Rwanda.CECAFA:TP Mazembe, DC Motema Pembe, AS Vita Club na Zesco United kushiriki Kagame Cup 2019 nchini Rwanda.AFCON 2019:Kundi A DR Congo,Misri, Uganda, Zimbabwe. Kundi B Burundi, Guinea, Madagascar, Nigeria. Kundi C Algeria, Kenya, Senegal, Tanzania. Kundi D Ivory Coast, Morocco, Namibia, Afrika Kusini. Kundi E Angola, Mali, Mauritania, Tunisia. Kundi F Benin, Cameroon, Ghana, Guinea-Bissau. CECAFA: Tanzania mwenyeji wa CECAFA Senior Challenge Cup 2019 Wanawake.CECAFA: Kenya mwenyeji wa CECAFA 2019 U-17 Wanawake. CECAFA: Uganda kuandaa CECAFA Senior Challenge Cup 2019.CECAFA::Eritrea kuandaa CECAFA Challenge Cup 2019 ya U-17.CECAFA:Rwanda mwenyeji CECAFA Kagame Cup 2019.CECAFA:Uganda mwenyeji CECAFA Challenge Cup 2019 ya U-20 Wanawake.

Ligi ya Taifa Handiboli Kenya kuendelea Alhamisi hii

Na Anthony Aroshee

Jumatano, Oktoba 9, 2019

Jumla ya mechi sita za ligi ya Taifa katika mchezo wa Mpira wa Mikono nchini Kenya zimeratibiwa kuchezwa siku ya Alhamisi hii kwenye Uwanja wa Kaloleni ulioko eneo bunge la Makadara Kaunti ya Nairobi.

Kwa mujibu wa ratiba ya ligi hiyo, mechi mbili za kwanza zitakuwa za Wanawake kabla ya kuchezwa mechi nyingine nne za Wanaume.

Mechi ya kwanza itawakutanisha timu za warembo ya National Youth Service NYS na Rising Starlets ambapo itaanza asubuhi saa 09:00hrs(EAT) kabla ya Mount Kenya University Thika MKU kupambana na mabingwa watetezi Nairobi Water.

Upande wa Wanaume, mpambano wa kwanza utakuwa kati ya Technical University of Kenya T.U.K na Nanyuki kisha Mount Kenya University Thika itakabana koo na timu ya Jomo Kenyatta University of Agriculture and Technology J.K.U.A.T huku Strathmore ivaane na St. Paul University SPU. Mechi ya mwisho Alhamisi hii ni baina ya Thika na Black Mamba.

Ligi hiyo itaendelea tena mwishoni mwa juma hili kwa mechi nyingine 12.

Na kuhusu matokeo ya mechi za ligi hiyo ya Taifa ya Mpira wa Mkono kwa Wanaume zilizofanyika Jumamosi iliyopita, timu ya Kaluluini ilikuwa na siku mbaya kwani ilipoteza mechi zake zote mbili. Kwanza ilifungwa na Thika mabao 35-21 kabla ya kulazwa tena na Inspired Boys mabao 42-19.

Nanyuki iliifunga Mount Kenya University Thika MKU mabao 37-35.

Rising Starlets iliichabanga Kaluluini mabao 36-19 wakati Bodmarang ilishinda mechi mbili dhidi ya timu za Warriors na Nanyuki kwa kuzifunga mabao 33-29.

Upande wa ligi ya Wanawake, Jumapili iliyopita, Kenyatta University Ladies iliichapa Rising Starlets mabao 31-24 huku Mount Kenya University Thika MKU ikipata ushindi wa bwerere wa mabao 15 na alama mbili bila kugusa mpira baada ya wapinzani wao National Youth Service NYS kukosa kufika Uwanjani Kaloleni.

Upande wa Wanaume vijana wa Inspired Boys waliishinda T.U.K kwa kuifunga mabao 17-13 ilhali timu ya St. Paul University SPU iliicharaza Thika mabao 40-28 huku Kenyatta University ikipata ushindi wa mabao 26-22 dhidi ya J.K.U.A.T.

Chapa Barua pepe

Share

Dula - Bila wewe

Kocha wa Bandari FC Twahir Muhidin