Yanayojiri

SOKA:Francesco Totti aachana na AS Roma kama mkurugenzi wa ufundi.CECAFA:Simba SC na Yanga SC zajiondoa kushiriki Kagame Cup 2019 nchini Rwanda.CECAFA:TP Mazembe, DC Motema Pembe, AS Vita Club na Zesco United kushiriki Kagame Cup 2019 nchini Rwanda.AFCON 2019:Kundi A DR Congo,Misri, Uganda, Zimbabwe. Kundi B Burundi, Guinea, Madagascar, Nigeria. Kundi C Algeria, Kenya, Senegal, Tanzania. Kundi D Ivory Coast, Morocco, Namibia, Afrika Kusini. Kundi E Angola, Mali, Mauritania, Tunisia. Kundi F Benin, Cameroon, Ghana, Guinea-Bissau. CECAFA: Tanzania mwenyeji wa CECAFA Senior Challenge Cup 2019 Wanawake.CECAFA: Kenya mwenyeji wa CECAFA 2019 U-17 Wanawake. CECAFA: Uganda kuandaa CECAFA Senior Challenge Cup 2019.CECAFA::Eritrea kuandaa CECAFA Challenge Cup 2019 ya U-17.CECAFA:Rwanda mwenyeji CECAFA Kagame Cup 2019.CECAFA:Uganda mwenyeji CECAFA Challenge Cup 2019 ya U-20 Wanawake.

Bandari kumjua mpinzani wake Jumanne hii Kombe la Shirikisho

Na Anthony Aroshee

Jumatano, Oktoba 9, 2019

Wawakilishi wa Kenya kwenye Michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, Bandari FC kutoka Mombasa Jumanne hii itamjua mpinzani wake katika kusaka kufuzu kwa hatua ya makundi ya mashindano hayo.

Shughuli ya kupanga timu katika makundi yaani droo ya hatua ya mechi za mchujo ya Kombe la Shirikisho Afrika inafanywa kuanzia usiku saa 20:00hrs(EAT) ya Jumanne hii ya Oktoba 9 jijini Cairo, Misri.

Timu 16 zilizoondolewa kwenye raundi ya kwanza ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika zitakutanishwa na timu 16 zilizotinga hatua ya mwisho ya mtoano ya Kombe la Shirikisho Afrika kupata idadi ya timu 16 ambazo zitatinga hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Timu hizo 16 zilizotolewa kwenye Ligi ya Mabingwa ni Yanga(Tanzania), UD Songo (Msumbiji), Côte d'Or (Ushelisheli), Green Eagles (Zambia), Fosa Juniors(Madagascar), Elect-Sport(Chad), KCCA(Uganda), Asante Kotoko(Ghana), FC Nouadhibou(Mauritania), Zamalek(Misri) ama Generation Foot(Senegal), Cano Sport(Guinea ya Ikweta), Gor Mahia(Kenya), ASC Kara(Togo), Horoya(Guinea) na Al Nasr(Libya).

Kwa mujibu wa Shirikisho la Soka Afrika CAF, Bandari FC imepangwa katika chungu cha mwisho(Chungu D) lenye timu za DC Motema Pembe (DR Congo), Triangle United (Zimbabwe), Bidvest Wits na TS Galaxy (Afrika Kusini), ESAE FC (Benin), FC San Pedro (Ivory Coast), Paradou (Algeria), Pyramids FC (Misri) na Proline (Uganda).

Kwa mujibu wa utaratibu wa kufanywa droo hiyo, Bandari inaweza kupangwa na moja ya timu kutoka chunga cha kwanza(Chungu A) ambacho kitakuwa na kundi la timu tisa (9) zilizotolewa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambazo ni Asante Kotoko (Ghana), Enyimba (Nigeria), Gor Mahia (Kenya), UD Songo (Msumbiji), Horoya (Guinea), KCCA (Uganda) na mshindi wa mechi baina ya Zamalek ya Misri na Generation Foot ya Senegal.

Chapa Barua pepe

Share

Dula - Bila wewe

Kocha wa Bandari FC Twahir Muhidin