Yanayojiri

Afcon Qualifier 2021:Kundi A: Namibia, Mali, Guinea, Chad. Kundi B: Uganda, Sudan Kusini, Malawi, Burkina Faso. Kundi C: Sudan, Ghana, Afrika Kusini, Sao Tome na Principe. Kundi D: Gambia, Gabon, DR Congo, Angola. Kundi E: Morocco, Mauritania, Jamhuri ya Kati, Burundi. Kundi F: Rwanda, Msumbiji, Cape Verde, Cameroon (mwenyeji). Kundi G: Togo, Kenya, Misri, Comoros. Kundi H: Zimbabwe, Zambia, Botswana, Algeria (Watetezi). Kundi I: Senegal, Guinea-Bissau, eSwatini (zamani Swaziland), Congo Brazzaville. Kundi J: Tunisia, Tanzania, Libya, Equatorial Guinea. Kundi K: Niger, Madagascar, Ivory Coast, Ethiopia. Kundi L: Sierra Leone, Nigeria, Lesotho, Benin.Afcon Qualifier 2021:Jumatano, Novemba 13, 2019. Namibia v Chad, Burkina Faso v Uganda, Malawi v Sudan Kusini, Sudan v Sao Tome na Principe, Angola v Gambia, Jamhuri ya Kati v Burundi, Cameroon v Cape Verde, Senegal v Congo Brazaville, Guinea-Bissau v E-eSwatini, Nigeria v Benin, Sierra Leone v Lesotho.. Afcon Qualifier 2021:Alhamisi, Novemba 14, 2019. Mali v Guinea, Ghana v Afrika Kusini, DR Congo, Msumbiji v Rwanda, Misri v Kenya, Togo v Comoros, Algeria v Zambia.Afcon Qualifier 2021:Ijumaa, Novemba 15, 2019. Morocco v Mauritania, Zimbabwe v Botswana, Tunisia v Libya, Tanzania v Equatorial Guinea.Afcon Qualifier 2021:Jumamosi, Novemba 16, 2019. Ivory Coast v Niger, Madagascar v Ethiopia.Afcon Qualifier 2021:Jumapili, Novemba 17, 2019. Guinea v Namibia, Chad v Mali, Uganda v Malawi, Sudan Kusini v Burkina Faso, Afrika Kusini v Sudan. CECAFA: Tanzania mwenyeji wa CECAFA Senior Challenge Cup 2019 Wanawake.CECAFA: Kenya mwenyeji wa CECAFA 2019 U-17 Wanawake. CECAFA: Uganda kuandaa CECAFA Senior Challenge Cup 2019.CECAFA::Eritrea kuandaa CECAFA Challenge Cup 2019 ya U-17.CECAFA:Rwanda mwenyeji CECAFA Kagame Cup 2019.CECAFA:Uganda mwenyeji CECAFA Challenge Cup 2019 ya U-20 Wanawake.

Warning: count(): Parameter must be an array or an object that implements Countable in /home/dawati/public_html/components/com_joomsport/models/default/ltable.php on line 63
EPL 2017-18

Msimu mpya wa ligi kuu ya England ya EPL mwaka 2017–18 utakuwa ni msimu wa 26 tangu ligi hiyo ianzishwe mwaka 1992. Msimu huu unaanza Ijumaa Agosti 11, 2017 na utakamilika Jumapili Mei 13, 2018. Ratiba ya ligi hiyo inayoshirikisha timu 20, ilitangazwa Jumatano Juni 14, 2017.

Chelsea ndio mabingwa watetezi.

Timu zilizopanda daraja msimu huu kutoka ligi ya  EFL Championship msimu uliopita wa 2016–17 ni Newcastle United, Brighton & Hove Albion na Huddersfield Town na kuchukua nafasi ya Sunderland, Middlesbrough na Hull City mtawalia. Timu hizo zilizoshushwa daraja sasa zitashiriki katika ligi ya EFL Championship msimu ujao wa 2017–18.

Timu ya Brighton & Hove Albion ilikuwa ya kwanza kupandishwa daraja na ilipata fursa hiyo baada ya kupata ushindi wa nyumbani wa mabao 2-1 dhidi ya Wigan Athletic Aprili 17, 2017 na kutoka sare na Huddersfield Town pamoja na Derby County bao 1-1 katika mechi za ligi ya EFL Championship msimu uliopita wa mwaka 2016–17.

Brighton & Hove Albion inacheza ligi ya daraja la juu zaidi nchini England kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1983, na inashiriki kwenye ligi kuu ya EPL kwa mara ya kwanza katika historia yao. Newcastle United ni timu ya pili kupanda daraja msimu huu na kurudi tena katika ligi hiyo baada ya kujikatia tiketi hiyo kwa kuifunga Preston North End mabao 4–1 nyumbani Aprili 24, 2017. 

Newcastle United ilitawazwa mabingwa Mei 7, 2017 wa ligi hiyo ya EFL Championship msimu uliopita wa mwaka 2016–17 baada ya kuichabanga Barnsley mabao 3–0 nyumbani na kutoa sare bao 1-1 dhidi ya Aston Villa na timu waliopandishwa nayo daraja pamoja ya Brighton & Hove Albion.

Huddersfield Town ni timu ya tatu kupanda daraja msimu huu ambayo iliifunga Reading mabao 4–3 katika mikwaju ya penalti baada ya dakika 90 kukamilika timu hizo zikitoshana nguvu kwa kutoka suluhu uwanjani katika mechi ya mchujo iliyofanyika Mei 29, 2017 kwenye ligi ya EFL Championship.

Huddersfield inacheza ligi ya daraja la juu zaidi nchini England kwa mara ya kwanza katika muda wa miaka 45, na inashiriki kwenye ligi kuu ya EPL kwa mara ya kwanza katika historia yao.

Nazo timu zilizoshushwa daraja baada ya kukamilika kwa msimu uliopita wa mwaka 2017-18 ni Sunderland, ambayo ilikuwa ya kwanza kuteremshwa daraja baada ya kufungwa nyumbani na AFC Bournemouth bao 1-0 Aprili 29, 2017. Sunderland imeshiriki katika ligi kuu ya EPL kwa muda wa miaka 10.

Middlesbrough ni timu ya pili kushuka daraja baada ya kupata kibano cha mabao 3-0 ugenini kwa Chelsea Mei 8, 2017. 

Nayo timu ya tatu kuteremshwa daraja ni Hull City ambayo pia ilijikuta ikishushwa daraja Mei 14, 2017 baada ya kufungwa ugenini mabao 4-0 na Crystal Palace ambayo ilisalia katika ligi kuu msimu huu.

Kipigo kwa Hull City kilisababisha Swansea City, ambayo pia ilikuwa katika tisho la kushuka daraja, kubaki kwenye ligi ya EPL msimu huu kutokana na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Sunderland.

Ligi hiyo ya EPL ina timu tano kutoka jiji la London; Arsenal, Chelsea, Crystal Palace, Tottenham na West Ham United. 

Timu nne zinazomaliza katika nafasi ya kwanza, huwa zinajikatia tiketi ya kuiwakilisha England kwenye michuani ya Klabu bingwa barani Ulaya huku timu tatu za mwisho, zinashushwa daraja. 

 

Pos
Timu
P W D L GD Pts
1 Manchester United 4 3 1 0 10 10
2 Manchester City 4 3 1 0 8 10
3 Chelsea 4 3 0 1 3 9
4 Watford 4 2 2 0 4 8
5 West Brom 4 2 1 1 0 7
6 Tottenham Hotspurs 4 2 1 1 4 7
7 Burnley 4 2 1 1 1 7
8 Huddersfield Town 4 2 1 1 2 7
9 Liverpool 4 2 1 1 0 7
10 Newcastle United 4 2 0 2 1 6
11 Arsenal 4 2 0 2 -1 6
12 Stoke City 4 1 2 1 0 5
13 Southampton 4 1 2 1 -1 5
14 Brighton & Hove Albion 4 1 1 2 -2 4
15 Swansea City 4 1 1 2 -3 4
16 Everton 4 1 1 2 -4 4
17 Leicester City 4 1 0 3 -2 3
18 West Ham United 4 1 0 3 -6 3
19 AFC Bournemouth 4 0 0 4 -7 0
20 Crystal Palace 4 0 0 4 -7 0


Warning: count(): Parameter must be an array or an object that implements Countable in /home/dawati/public_html/components/com_joomsport/views/ltable/tmpl/default.php on line 328

Share

Powered by OrdaSoft!

Dula - Bila wewe

Kocha wa Bandari FC Twahir Muhidin