Yanayojiri

SOKA:Francesco Totti aachana na AS Roma kama mkurugenzi wa ufundi.CECAFA:Simba SC na Yanga SC zajiondoa kushiriki Kagame Cup 2019 nchini Rwanda.CECAFA:TP Mazembe, DC Motema Pembe, AS Vita Club na Zesco United kushiriki Kagame Cup 2019 nchini Rwanda.AFCON 2019:Kundi A DR Congo,Misri, Uganda, Zimbabwe. Kundi B Burundi, Guinea, Madagascar, Nigeria. Kundi C Algeria, Kenya, Senegal, Tanzania. Kundi D Ivory Coast, Morocco, Namibia, Afrika Kusini. Kundi E Angola, Mali, Mauritania, Tunisia. Kundi F Benin, Cameroon, Ghana, Guinea-Bissau. CECAFA: Tanzania mwenyeji wa CECAFA Senior Challenge Cup 2019 Wanawake.CECAFA: Kenya mwenyeji wa CECAFA 2019 U-17 Wanawake. CECAFA: Uganda kuandaa CECAFA Senior Challenge Cup 2019.CECAFA::Eritrea kuandaa CECAFA Challenge Cup 2019 ya U-17.CECAFA:Rwanda mwenyeji CECAFA Kagame Cup 2019.CECAFA:Uganda mwenyeji CECAFA Challenge Cup 2019 ya U-20 Wanawake.

Kenya

‘Waasi’ wa Ganjoni waiua Mombasa Sports Club.

 

Na Anthony Aroshee

Alhamisi Julai 30, 2015

Mabao mawili yaliyotumbukizwa wavuni na Said Suleiman, yaliiwezesha klabu ya Ganjoni Rebels kuifunga timu ya Mombasa Sports Club(MSC) mabao 2-1 katika mechi ya ligi ya Mombasa Premier iliyopepetwa kwenye uwanja wa Mombasa Sports Club(MSC) siku ya jumatano Julai 29, 2015.

Soma Zaidi

Chapa Barua pepe

Shimo la Tewa FC wanaomba mechi zao zihairishwe.

 

 

Na Anthony Aroshee

Jumamosi Julai 18, 2015

Klabu ya Soka ya Shimo la Tewa, inayoshiriki katika ligi ya Taifa daraja la kwanza nchini Kenya, imeiandikia barua meme shirikisho la Kabumbu nchini humo FKF ya kuliomba Shirikisho hilo kuaihirisha mechi zao za mwishoni mwa juma hili hadi mwezi ujao wa Agosti kutokana sababu za kiusalama.

Soma Zaidi

Chapa Barua pepe

Shule ya msingi ya Maryango ndio mabingwa wa michuano ya MTG kwa shule za msingi Kilifi nchini Kenya.

 

Na Anthony Aroshee

Ijumaa Julai 17, 2015

Shule ya msingi ya Maryango ilitwaa ubingwa wa michuano ya kombe la MTG kwa shule za msingi katika Kaunti ya Kilifi nchini Kenya baada ya kuishinda shule ya msingi ya Kawala mabao 3-2 katika mchezo wa fainali iliyochezwa kwenye uwanja wa Karisa Maitha mjini Kilifi.

Soma Zaidi

Chapa Barua pepe

Polisi wazima ‘Swichi’ ya Stima nchini Kenya.

 

Na Anthony Aroshee

Ijumaa Julai 17, 2015

Timu ya Soka ya ‘Maafande’ ya Kenya Police ya kutoka Kaunti ya Nairobi walishinda ugenini kwa kuifunga ‘Wasambaza nguvu za Umeme’ Coast Stima FC ya kutoka Kaunti ya Mombasa mabao 2-1 katika mpambano wa FKF Supaligi ya Taifa nchini Kenya, iliyopepetwa kwenye uwanja wa Kaunti ya Mombasa nchini humo.

Soma Zaidi

Chapa Barua pepe

Tononoka Sekondari yajiandaa kwa mashindano ya mkoa nchini Kenya.

 

Na Anthony Aroshee

Jumanne Julai 7, 2015

Mabingwa wa Soka kwa shule za upili za wavulana katika kaunti ya Mombasa nchini Kenya, wamefanya mazoezi yao ya mwisho asubuhi ya siku ya jumanne Julai 7, 2015 kwenye uwanja wa Bomani kwa maandalizi ya kushiriki kwenye mashindano ya jimbo la pwani nchini humo.  

Soma Zaidi

Chapa Barua pepe

Ligi ndogo ya mkoa FKF tawi la Pwani Kaskazini nchini Kenya kuanza ijumaa

Mechi za ligi ndogo katika Shirikisho la Soka nchini Kenya (FKF) Tawi la Pwani Kaskazini, zitaanza kuchezwa kuanzia siku ya ijumaa na kukamilika jumapili mwezi huu wa Novemba mwaka 2014.

Timu nane ambazo zimegaanywa katika makundi mawili, ndizo zilizofuzu baada ya kushiriki kwenye ligi ya mkoa ya tawi hilo la pwani kaskazini mwaka 2014.

Katika kundi A kuna Gongoni FC, Kilifi Gold FC, Wesa United FC na Zambarani FC wakati kwenye kundi B kumeorodheshwa BlackStars FC, Mission Boys FC, Rocky Stars FC na Tezo Stars FC.

Endelea kusoma

Chapa Barua pepe

Njuguna Joseph ni kipa mwenye ujasiri langoni.

 

Na Francis Mudzo

Jumatano Januari 6, 2016

Ni golikipa wa kupigiwa mfano na anayekuja kwa kasi ya kutisha kwenye eneo la kaunti ndogo ya Mwihoko katika kaunti ya Kiambu nchini Kenya huyu sio mwengine ila Njuguna Joseph mwenye umri wa miaka 15 anayetoa huduma zake kwa kituo cha kukuza soka ya vijana ya Changes Soccer Academy.

Soma Zaidi

Chapa Barua pepe

Kombe la Kagame: Mechi za nusu fainali kuchezwa ijumaa.

 

Na Victor M. Abuso, akiwa Dar es Salaam 

Alhamisi Julai 30, 2015

Vipute vya nusu fainali ya michuano ya nusu fainali kuwania ubingwa wa soka baina ya vilabu vya nchi za Afrika Mashariki na Kati CECAFA, inachezwa Ijumaa hii Julai 31 kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam nchini Tanzania.

Soma Zaidi

Chapa Barua pepe

Sparki Youth yapata ushindi wa ‘Chee’ nchini Kenya.

 

Na Anthony Aroshee

Ijumaa Julai 17, 2015

Klabu ya Soka ya Sparki Youth ilipata ushindi wa bwerere wa alama tatu na mabao mawili bila kugusa mpira baada ya wapinzani wao timu ya Green Berrets waliokuwa wachuane nao katika mechi ya FKF Supaligi ya Taifa NSL nchini Kenya kutofika kwenye uwanja wa Kaunti ya Mombasa. 

Soma Zaidi

Chapa Barua pepe

Ligi Ndogo ya mkoa tawi la Pwani Kaskazini kuanza

FKF

Shirikisho la Soka la Kenya (FKF) Tawi la Pwani Kaskazini limepanga mechi za ligi ndogo kuanza ijumaa ya tarehe 28 mwezi Novemba hadi jumapili ya tarehe 30 mwezi Novemba mwaka 2014.

Timu nane ndizo zilizofuzu baada ya kupambana katika ligi ya mkoa ya mwaka 2014 ambazo ni Gongoni FC, Tezo Stars FC, Wesa United FC, Zambarani FC, BlackStars FC, Kilifi Gold FC, Rocky Stars na Mission Boys. 

Tezo Stars FC ndiyo iliyoongoza katika kundi la B kwa alama 39, alama mbili zaidi ya Wesa United FC iliyomaliza katika nafasi ya pili. Kilifi Gold ilikuwa ya tatu kwa kuambulia alama 31. 

Kwa mujibu wa katibu mkuu wa shirikisho la FKF tawi la Pwani Kaskazini Raphael K. Mwalungo, mechi za ligi hiyo ndogo zitachezwa kwenye uwanja wa shule ya upili ya Malindi. Timu itakayofanya vema, itafuzu kushiriki katika supaligi ya Taifa inayoandaliwa na shirikisho la soka nchini, FKF mwakani 2015.

Chapa Barua pepe

Share

Powered by OrdaSoft!

Dula - Bila wewe

Kocha wa Bandari FC Twahir Muhidin