Yanayojiri

Afcon Qualifier 2021:Kundi A: Namibia, Mali, Guinea, Chad. Kundi B: Uganda, Sudan Kusini, Malawi, Burkina Faso. Kundi C: Sudan, Ghana, Afrika Kusini, Sao Tome na Principe. Kundi D: Gambia, Gabon, DR Congo, Angola. Kundi E: Morocco, Mauritania, Jamhuri ya Kati, Burundi. Kundi F: Rwanda, Msumbiji, Cape Verde, Cameroon (mwenyeji). Kundi G: Togo, Kenya, Misri, Comoros. Kundi H: Zimbabwe, Zambia, Botswana, Algeria (Watetezi). Kundi I: Senegal, Guinea-Bissau, eSwatini (zamani Swaziland), Congo Brazzaville. Kundi J: Tunisia, Tanzania, Libya, Equatorial Guinea. Kundi K: Niger, Madagascar, Ivory Coast, Ethiopia. Kundi L: Sierra Leone, Nigeria, Lesotho, Benin.Afcon Qualifier 2021:Jumatano, Novemba 13, 2019. Namibia v Chad, Burkina Faso v Uganda, Malawi v Sudan Kusini, Sudan v Sao Tome na Principe, Angola v Gambia, Jamhuri ya Kati v Burundi, Cameroon v Cape Verde, Senegal v Congo Brazaville, Guinea-Bissau v E-eSwatini, Nigeria v Benin, Sierra Leone v Lesotho.. Afcon Qualifier 2021:Alhamisi, Novemba 14, 2019. Mali v Guinea, Ghana v Afrika Kusini, DR Congo, Msumbiji v Rwanda, Misri v Kenya, Togo v Comoros, Algeria v Zambia.Afcon Qualifier 2021:Ijumaa, Novemba 15, 2019. Morocco v Mauritania, Zimbabwe v Botswana, Tunisia v Libya, Tanzania v Equatorial Guinea.Afcon Qualifier 2021:Jumamosi, Novemba 16, 2019. Ivory Coast v Niger, Madagascar v Ethiopia.Afcon Qualifier 2021:Jumapili, Novemba 17, 2019. Guinea v Namibia, Chad v Mali, Uganda v Malawi, Sudan Kusini v Burkina Faso, Afrika Kusini v Sudan. CECAFA: Tanzania mwenyeji wa CECAFA Senior Challenge Cup 2019 Wanawake.CECAFA: Kenya mwenyeji wa CECAFA 2019 U-17 Wanawake. CECAFA: Uganda kuandaa CECAFA Senior Challenge Cup 2019.CECAFA::Eritrea kuandaa CECAFA Challenge Cup 2019 ya U-17.CECAFA:Rwanda mwenyeji CECAFA Kagame Cup 2019.CECAFA:Uganda mwenyeji CECAFA Challenge Cup 2019 ya U-20 Wanawake.

Voliboli

Msimu mpya wa ligi kuu ya Voliboli nchini Kenya kuanza

Na: DLM

Shirikisho la mchezo wa mpira wa Wavu nchini Kenya, KVF limetoa ratiba ya mechi za mkondo wa kwanza za msimu mpya wa ligi kuu nchini humo itakayofanyika mjini Nakuru kuanzia wikendi ya Februari 27 mwaka huu 2015.

Ligi hiyo ya wanawake na wanaume ambayo itadhaminiwa na kampuni ya Kenya Pipeline, inatarajiwa kuwa ngumu kutokana na kuongezeka kwa udhamin mnono.

Endelea kusoma

Chapa Barua pepe

Al Ahly mabingwa Voliboli Klabu Bingwa Afrika

Na Dawati la Michezo

Jumatatu, Aprili 09, 2018

Wenyeji klabu ya Al Ahly ya Misri walilihifadhi tena taji lao baada ya kuishinda klabu ya El Guish na kutangazwa mabingwa kwa mara ya 13 Michuano ya Klabu Bingwa Barani Afrika katika mchezo wa Mpira wa Wavu mwaka huu 2018, Upande wa Wanaume.

Endelea kusoma

Chapa Barua pepe

Kinadada Wang'ara Katika Timu ya Wanawake Bomu

KINA Dada wameanza kujitokeza katika Nyanja mbali mbali za michezo humu nchini ikizingatiwa kwamba michezo kama vile soka, riadha na mingineyo ni ajira.

Timu ya wasichana ya Bomu Ladies ni timu ya kina dada ya Voliboli ambayo imejitokeza kuonyesha kuwa wanawake wanaweza kufanya kile wanaume hufanya. Ni timu iliyoanzishwa mapema mwaka 2008 katika eneo la Bomu wilayani Changamwe katika jimbo la Mombasa katika Pwani ya Kenya na mkufunzi George Amolo maarufu “Papaa” baada ya kuona vipawa vilivyo kuwa viking’ara kwenye shule mbali mbali vikiyeyuka bila mafanikio.

Kocha George “Papaa” alianza kuwakusanya kina dada waliokuwa wakichezea timu za shule mbali mbali katika wilaya ya Kisauni na kuunda timu hiyo ambayo kwa sasa imekuwa tishio kwa timu zingine mkoani pwani. Timu hiyo kwa sasa ina idadi ya wachezaji 23 ambao kila mmoja anajiamini wanapokuwa uwanjani. 

Mkufunzi huyo alisema kuwa, kutokana na kuwa mitaa mingi imegubikwa na wimbi la utumizi wa dawa za kulevya na visa vingine viovu katika jamii, alionelea kuwaweka pamoja kina dada hao. Baadhi ya wachezaji ambao wapo kwenye kundi hilo ni Saida Swaleh ambaye ndiye nahodha Rehema Bakari naibu nahodha Grace Githaiga, Cate Ondero, Regina Kirimi, Everline Chepoghiso na Nancey Chepchirichir.

Wengine ni Emmily Ndanu, Edith Sewe, Essy Kanana, Max Chepchirichir na Florence Maina.

Kina dada hao walionyesha uwezo wao wa kucheza mchezo huo kwa umakini sana pale waliposhiriki kwenye michuano ya kipute cha kuwania taji la Mududa Waweru Cup lililofanyika katika eneo hilo la Changamwe.

Bomu Ladies waliweza kuwafunga majirani zao Bokole Ladies seti 3-1 za 25-16, 24-26, 25-21 na 25-18. Katika mechi nyingine, Bomu Ladies walilemewa na Migadini Ladies seti 3-2 za 25-23,11-25, 25-22, 10-25 na 15-11.Licha ya wakufunzi wengi kujitahidi kuona kwamba wanalea na kuinua vipawa vya vijana, mitaani bado changamoto ni uwezo wa kujisimamia kifedha kwa ajili ya usafiri na vifaa vya kimchezo.

Kocha “Papaa” alisema kuwa kuna uwezekano wa timu za mashinani kutoa wachezaji bora na kufanya vyema katika mechi za kitaifa lakini umasikini na kukosa udhamini ndio hudidimiza matumaini ya wengi. “Papaa” alimtaja Blasto Ooto kuwa mfano wa kuigwa na watu wengi pamoja na makampuni kwani amekuwa msaada mkubwa kwa timu hiyo ya kina dada.

Hata hivyo amewataka wahisani na wenye makampuni kuekeza katika michezo kwa ajili ya kuinua vipawa vya vijana.

Chapa Barua pepe

Share

Powered by OrdaSoft!

Dula - Bila wewe

Kocha wa Bandari FC Twahir Muhidin